KONA YA SHERIA: HAKI ZA MTUHUMIWA MBELE YA POLISI 0 comments1. Mtuhumiwa ni nani?
Ni mtu yeyote ambaye anawekwa chini ya ulinzi na
polisi au chombo cha usalama kwa kutuhumiwa
kufanya kosa la jinai.
2. Makosa ya jinai ni yapi?
Ni makosa ambayo mtu akipatikana na hatia hupe-
wa adhabu.
Ni makosa kama wizi, ubakaji, mauaji, kufanya
makosa ya kuhatarisha amani n.k.
3. Haki za Mtuhumiwa
(a) Mtuhumiwa anapowekwa chini ya ulinzi
ana haki ya kuelezwa sababu za kukamatwa
au kutiliwa mashaka.
(b) Mtuhumiwa ana haki ya kudai risiti ya orodha
ya vyombo/mali atakayokuwa nayo wakati
wa kumpekua zile zinazochukuliwa kituoni na
pale anapokabidhiwa polisi.
(c) Mtuhumiwa akiwa mwanamke lazima
kukaguliwa na polisi mwanamke.
(d) Mtuhumiwa ana haki ya kudai kibali cha
hakimu pale majadiliano/maelezo kwa polisi
yanapozidi saa nane.
(e) Mtuhumiwa anayo haki ya kudai awasiliane na
mtu anayemtaka akiwa chini ya ulinzi.
Kwa mfano rafiki, ndugu au wakili.
(f) Mtuhumiwa ana haki ya kufikishwa
mahakamani katika muda usiozidi masaa 24.
(g) Mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya wakati
wa mahojiano na polisi na anapaswa kuelezwa
kwamba chochote ambacho mtuhumiwa
atawaeleza polisi inaweza kutolewa
mahakamani kama ushahidi dhidi yake.
(h) Mtuhumiwa ana haki ya kutojibu maswali
ya polisi na kukaa kimya hadi polisi
anayemuuliza/endesha mahojiano awe
amemueleza mtuhumiwa yafuatayo:
(i) cheo alicho nacho na jina lake
(ii) mtahadharishwa kwamba yuko chini ya ulinzi.
(iii) kosa alilofanya au sababu ya kuwa chini ya ulinzi.
(iv) anayo haki ya kudai asomewe kilichoandikwa
kabla ya kuweka sahihi kwenye maelezo.
Mtuhumiwa anayo haki ya kupewa heshima na
kuthaminiwa kwamba ni binadamu. Hakuna ruhusa
kumtesa mtuhumiwa na kumdhalilisha anayo haki
ya kudai matibabu.
(i) Mtuhumiwa anaweza akaomba dhamana wakati
yuko chini ya ulinzi wa polisi.

Imeandaliwa na: Paul Chengula(mgodi unaotembea) 
Kwa maelezo zaidi juu ya tatizo la kisheria ulilo nalo au unahtaji sheria(ACT) yeyote ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,wasiliana nami kwa 0755334530 au paulchengula@gmail.com

Mafuriko Dar es salaam,hapakaliki,watu 13 wafariki,mvua kuendelea kwa siku mbili zijazo 0 comments

21 december 2011
Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar zimesababisha mafuriko na kusababisha mamia ya watu kukosa makazi na habari zilizopo ni kuwa idadi ya watu wapatao 13 wamefariki dunia,na eneo lililo athirika zaidi ni Jangwani maeneo mengine ni Tandare,Tabata,Mbezi kibanda cha mkaa n.k,habari kutoka hali ya hewa zinadai mvua hizo zinaweza kuendelea siku mbili zijazo,hivyo wakazi wa kwenye maeneo husika kama mabondeni kuombwa kuchukua tahadhari
Hili ni eneo la Jangwani
watu wanajiokoa
mafuriko
na barabara imezuiwa
bado hali ni tete Dar
gari hatarini

Gari likijaribu kukatiza

Eneo la jangwani

WALIOFUKUZWA CHUO KIKUU UDSM KUKATA RUFAA,CHADEMA NAYO YATOA TAMKO 1 comments

17 novemba 2011
picha na maktaba yangu:wanafunzi UDSM wakiandamana
Baadhi ya wanafunzi waliofukuzwa UDSM wana mpango wa kukata rufaa kutokana na hukumu waliyopewa na uongozi wa chuo hicho,wakiongea na waandishi wa habari ikiwemo star tv wanafunzi hao wanasema watakata rufaa ili kuwezeshwa kuendelea na masomo chuoni hapo,baadhi ya wanafunzi hao wamesema utawala wa chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) haukuwatendea haki ya kikatiba ya kutokusikilizwa,wakiongea baadhi ya wanafunzi hao wamesema hawako tayari kuomba radhi kwani wanajua walichokuwa wanapigania kilikua ni cha kweli na cha msingi, wanafunzi hao wamefutiwa udahili ktk chuo kikuu cha Dar(UDSM) baada ya kufanya mgomo kwa madai ya kupewa mikopo wenzao wa mwaka wa kwanza mapema mwezi wa novemba


Chadema yapinga kuhusika na migomo vyuo vya elimu ya juu
Wakati hayo yakiendelea chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kimepinga shutuma zinazoletwa juu yake kuhusika na migomo vyuoni kama baadhi ya watu ambavyo husema,akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho Bwana Heche amesema,msingi wa tatizo lote ni bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo kila siku imekuwa ikilalamikiwa kuwa ndio chanzo cha matatizo,so serikali inabidi iwe makini katika kushughulikia masuala yanayohusu wanafunzi wa elimu ya juu na si kukimbilia kuwafukuza kwa tatizo ambalo chanzo chake kinaeleweka ni bodi ya mikopo!

TANZANIA NI NCHI YA TATU DUNIANI KWA KUOMBA MISAADA 0 comments

KONA YA UCHUMI
Waziri wa Fedha na uchumi Tanzania mh:Mstapha Mkulo
 
Tanzania imekua nchi ya tatu duniani katika kuomba misaada ya maendeleo (official development assistance)baada ya Irak na Afghanistan ambazo zinaongoza katika mtiririko huo,Afrika ina nchi 12 zilizo 20 bora duniani kwa kuomba misaada,nchi ya Marekani ndio inayoongoza kwa kutoa misaada ikifuatiwa na ujerumani na ufaransa,nimeona nisiifaidi peke yangu ripoti hii nawe sasa jisomee mwenyewe hapa:

"Tanzania, whose aid portfolio has ballooned to over Sh3 trillion (about $2.89 billion) in its 50 years of independence, is currently Africa’s top beggar for development assistance, The Citizen on Sunday can authoritatively report today.That level of dependency makes it the third leading recipient of official development assistance (Oda) in the world after war-torn Iraq and Afghanistan.

The American organisation Visual Economics says the once-rich oil exporter Iraq tops the list of beggar nations with donations totalling about $9 billion followed by Afghanistan and Tanzania, whose development alms are nearly $4 billion and $3 billion, respectively, according to 2010 figures.

But the government yesterday questioned the accuracy of the report, saying there were many other countries that received much more in foreign assistance than Tanzania. Finance and Economic Affairs deputy permanent secretary Servacius Likwelile told The Citizen on Sunday that countries like Israel and Egypt receive a substantial amount of assistance from the US annually, and wondered whether the report included military aid.

“We need to know the criteria used in compiling the report. What I know is that the United States provides a great deal in assistance to countries such as Israel and Egypt, but they are not even on the list,” Dr Likwelile said.Commenting on the trend, some experts said that while begging for the top two is understandable, it is incomprehensible for Tanzania, which is not only rich in both natural resources and human capital, but has also been stable and peaceful since independence.

They wondered why, despite the staggering amounts of aid the country has been receiving for five decades, the country remains one of the poorest in the world with a third of the population living below the poverty line.

Some attributed the limited value for money on aid to bad governance, a view supported by the 2009 Human Rights Report, which states that “senior government officials estimated that 20 per cent of the government’s budget in each fiscal year was lost to corruption”.

“We are still poor despite being among the top recipients of aid in the world…this is because of poor leadership and management of the aid provided. Worst of all, we are poor managers of our God-given resources,” said Ms Saumu Jumanne, a lecturer at the Dar es Salaam University College of Education.

Saying Tanzania could forge ahead without aid, she added that foreign assistance has not helped to alleviate poverty as only a trickle reaches the targeted groups. Sometimes, she noted, even aid for orphans is misappropriated.

“What is needed is to make strategic plans and be focused on exploiting our immense natural resources for the public good. So far, the abundant natural resources we have benefit a few Tanzanians and their foreign partners. Our education, which is supposed to guide us in transforming our nation, is grossly inadequate.

Agriculture is not being taught at primary level yet 85 per cent of the populace depends on the sector for survival. That is having our priorities wrong.”

Economist Honest Ngowi said foreign aid has not made Tanzania economically independent because the dynamics of the Oda industry are not geared at ending the dependency syndrome. He blames both donors and the authorities for aid’s failure to address the country’s development shortcomings, saying he does not foresee an end to the vicious circle of begging in the near future.But Dr Likwelile differed with this point of view, saying foreign aids had made “a lot of difference” in the water, education and health sectors.

Visual Economics, which claims to be the world leader in unravelling complexities of economic and financial data, says Africa has five of the world’s top 10 aid recipients, Asia four and the Middle East one. Using data obtained from the Organisation of Economic Cooperation and Development (OECD) sources, it shows that Africa has 12 of the top 20 development assistance beggars in the world.

“The top recipient of developmental aid is Iraq, with $9.115 billion in donations. Number two is Afghanistan, with $3.951 billion in donations received. Number three is Tanzania, with $2.811 billion received in donations. Number four is Vietnam, with $2.497 billion in donations,” Visual Economics notes in a publication titled How Developmental Aid Flows Around The Globe.

“Number five is Ethiopia, with $2.422 billion in donations. Number six is Pakistan, with $2.212 billion in aid received. Number seven is Sudan, with $2.104 billion in aid received. Number eight is Nigeria, with $2.042 billion in donations received. Number nine is Cameroon, with donations of $1.933 billion received. Number 10 is Palestine with $1.868 billion in donations received,” it adds.

The US is the number one developmental aid donor with $21.787 billion donated followed by Germany and France, which donated $12.291 billion and $9.884 billion, respectively. Despite close relations between Tanzania and the US, the country is not on the list of the top 10 recipients of American aid. Topping the list are Iraq ($4.266 billion) and Afghanistan ($1.459 billion).

According to the OECD figures, Tanzania received about $39 million (about Sh66.3 billion at current exchange rates) in foreign aid in 1961, but the amount surged to about $2.89 billion (about Sh4.91 trillion) in 2009. In terms of sectoral distribution, most of the aid in the 1960s and the early 1970s was channelled to the agricultural and transport sectors.

During the second half of the 1970s, the emphasis shifted to industry and energy. Transport became an important aid recipient in the late 1980s and early 1990s. The general pattern of aid distribution since the 1990s has been (in order of importance) transport and communications, followed by agriculture, human resources development, health, integrated regional development and ener
gy".

Source:the citizen on sunday

JERRY MURO AACHIWA HURU NA MAHAKAMA 0 comments

Jarry muro akiwa na mke wake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru
Muro akionge na waandishi wa habari baada ya kushinda kesi
30 november 2011
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaachia huru kwa mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na wenzake wawili.

Hakimu Frank Moshi, alisema anawaachia washitakiwa hao kwasababu upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi shaka.

Muro, Edmond Kapama pamoja na deogratius Mgasa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage.

Mashitaka yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.

Muro baada ya kutoka mahakamani alitangaza kwa wanahabari kuwasamehe wabaya wake wote ambao ni viongozi wa serikali baadhi na baadhi ya maafisa wa polisi na kuwataka waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo unaoendelea bila woga.

Katika hukumu, hakimu Moshi alisema baada ya kuangalia ushahidi mahakama ilikuwa na maswali ya kujiuliza kama upande wa jamuhuri uliweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa ambapo shitaka la kula njama kwa nia ya kuomba rushwa ambalo linawahusu washitakiwa wote, ushahidi ulikuwa wa Wage.

Shahidi huyo wa tatu wa jamuhuri lisema alikutana na Muro kwenye mgahawa wa Califonia ambapo mawasiliano kati yao yaliendelea kwa njia ya simu ya mkononi. 

Ushahidi huo ulikuwa hafifu kwasababu upande wa mashitaka haukuweza kuwasilisha karatasi ya mawasiliano kati yao kutoka kwenye kampuni ya mtandao wa simu (printout).

Vile vile alisema picha za CCTV iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa ni kivuli kisichoonyesha sura za watu badala yake wangeleta CD kuonyesha kwenye video ili watu waweze kutambulika kwa urahisi. 

Mawasiliano ni jambo la msingi kwasababu ili kula njama ni lazima mawasiliano yafanyike hivyo kuna mapungufu makubwa katika shitaka hilo.

Dereva aliyemwendesha wa Wage alidaiwa kuwa na Wage pale mgahawa wa Califonia walipokutana na Muro, alitakiwa kuletwa athibitishe kama Wage na Muro walikutana upande wa mashitaka hawakumwita shahidi huyo.

Katika shitaka la kuomba rushwa lilowakabili wote katika ushahidi wake Wage, alieleza Muro na wenzake walimtaka awapatie Sh milioni 10 watamsaidia kwenye tuhuma zinazomkabili lakini hakuwa nazo akawapa sh milioni moja mbali na ushahidi huo hakuna ushahidi mwingine wa serikali unaoonyesha kuwa walipokea fedha hiyo.

“Mahakama ilitegemea kuwe na ushahidi wa mawasiliano kama haupo wa kuona lakini hayo yote hayakufanyika,” alisema hakimu Moshi.

Muro alikamatwa ndani ya gari, mahakama haielewi ni kwanini kulikuwa na haraka hiyo kwanini asingeachwa wakakutana na Wage. Kwa upande wa hotel ya Sea Cliff ni sehemu ya watu yoyote anaweza kwenda.

Washitakiwa Mgasa na Kapama hakimu Moshi alisema hawakukamatwa eneo la tukio walikamatwa na kuunganishwa na halikufanyika gwaride la kuwatambua na cheti kuletwa mahakamani.

Shitaka la linalowakabili Mgasa na Kapama la kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU mahakama ilisema halikuthibitishwa lina mashaka. Alisema washitakiwa walijitambulisha kwa moja anaitwa Dr na mwingine Musa.

Upande wa mashitaka ulitakiwa kufatilia mtaani kama majina hayo washitakiwa walikuwa wakiyatumia lakini hilo halikufanyika.

“Wage kama msomi ngazi ya uhasibu aliwezaje kukubali mtu ajitambulishe kwa mdomo kama afisa wa TAKUKURU bila kuonyeshwa vitambulisho na akakubali mahakama inapata mashaka”. 

Aliongeza hakimu huyo hakuna vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha bila kuacha shaka hivyo wanaachiwa huru kwa mashitaka yote.

Alisema Moshi risiti, pingu na miwani havikuwa na mgogoro katika kesi na kwavile vilipatikana kwa risiti basi arudishiwe muhusika na upande unataka kukata rufaa wana ruhusiwa. Wakili kiongozi wa kesi hiyo Boniface Stanslaus alisema taafifa atampelekea Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ataamua kama watakata rufaa.

Washitakiwa walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mkazi, Gabriel Mirumbe.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA LEO 0 comments

27 november 2011

Viongozi waandamizi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wakitafakari kabla ya kikao
viongozi wa CHADEMA wakisalimiana na waziri Bernard Membe
Hapa wakipata picha ya pamoja
Mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu akisalimiana na waziri Lukuvi
Raisi kikwete anaongea jambo na Prof Baregu Mwesiga
Raisi kikwete akisalimiana na John Mnyika

Hapa Raisi akimkaribisha mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe

SIR ALEX FERGUSON WA MAN U ASHANGAA MAAMUZI YA REFA JUU YA PENALT 0 comments

26 NOVEMBER 2011
Sir Alex Ferguson ameshindwa kuficha hisia zake juu ya droo aliyotoka na Newcastal leo,Man U ambao waliongoza mapema tu kunako second half kupitia kwa mchezaji Javier Hernandez,lakini baadaye goli hilo lilisawazishwa na Newcastal kupitia kwa Demba Ba kwa mkwaju wa penati, Sir Alex anaamini kuwa refaree Mike Jones hakutakiwa kumsikiliza msaidizi wake na hakutegemea maamuzi yale, anasema "kila mtu pamoja na refaree walishangaa so haikutakiwa iwe penati in short it was not fair" ameongezea ferguson kama alivyoongea na waandishi wa habari kuwa
"Everyone, including the referee, was astounded. He was put in a terrible position. Why can't the referee overrule it when he is only eight yards away?"
"The problem is that the referees are full-time and the linesmen are not, and whether he ever gets a game again, the assistant referee, is not for me to decide but it was an absolutely shocking decision" unaona ee..........!

HOFU YATANDA LIVERPOOL “Gerlad kutocheza mechi ya jumapili na Mancity” 1 comments

 24 november 2011


Steven Gerrard atakosa kucheza mechi ya jumapili na mancity na bado haijaeleweka ni lini mchezaji huyo ataweza kurudi tena uwanjani, wakati huohuo boss wa majogoo hao (Liverpool) Kenny Dalglish ameendelea kusisitiza kua anafurahia maendeleo ya Gerlad baada ya matibabu,lakini hakua tayari kuelezea ni lini Kaptein huyo  atarudi tena uwanjani
Kenny Dalglish amesema kuwa kila mchezaji atakuwepo katika mechi ya jumapili isipokuwa Gerlad na Jack Robinson.
Namnukuu Kenny Dalglish kama alivyokua anaongea na waandishi kama ilivyoonyeshwa na Sky Newz
“Like we've already said, we are delighted with the progress he's making and we've said that we won't put a date on his return - and we won't put a date on it now”

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAFA KWA AJALI 0 comments

20 november 2011


(Moses Mwale (Zambian) mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyesalimika kati ya kumi, watatu wamelaza Hospitali ya Ngara.)


Ajali ya Basi la Taqwa na Lori la Azam iliyotokea jana Lusaunga wilaya ya Biharamulo imeteketeza wanafunzi 6 wa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa wakichukua Masters of Science in Mathematical Modelling, walikuwa wakienda Rwanda kwenye warsha ya Pure Mathematics.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Kozi hiyo yenye wanafunzi toka mataifa mbalimbali katika UDSM Dk Wilson Manera Charles alisema wanafunzi hao ni kati ya kumi ambao waliteuliwa kuwakilisha katika warsha hiyo ya wanahisabati inayofanyika kila mwaka, wannne wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu, aliongeza kuwa waliokufa ni Mzambia mmoja, Malawi 2, Mganda 1 na Watanzania 2.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya alisema vimeongezeka vifo 2 na kufikia jumla 18 na kuwa mpaka sasa maiti zote zimetambuliwa na nane kuchukuliwa na ndugu zao kwa maziko, mingine insaburi ndugu.
Pia aliongeza kuwa Mtoto mdogo wa kiumu anayekadiriwa kuwa na miaka miwili na nusu ambaye mama yake amefariki ajalini amehamishiwa hospitali ya Bugando Mwanza kwa matibabu zaidi.
Majeruhi walioko Biharamulo ni Tina Elisha, Rose Nula, Janet Kisanga, Moses Mwale, Joseph Bigilimana, Anicet Mrundi, Joseph Baltazary na Masalu Leonard.
Maiti zilizotambuliwa ni Abiba Juma, Faida Abdalah, Aziza Said, Andi Ibrahim, Chanda Congo, Nshaija Muganyizi na Kasimu Dadi, wengine ni Erick Eliude, Chinuka Hamajata na Ndizeye Pili.kwa habari kama hizi na nyingine nyingi usikose kutembelea blog hii!

KONA YA BURUDANI: IDA MREMBO MTANZANIA ANEYEJIVUNIA KUPIGA PICHA ZA UTUPU 1 comments

Mwanamitindo Mtanzania, Ida Ljungqvist amesema kuwa ataendelea kupiga picha za X kwa sababu zinampa utajiri.
Ida mwenye maskani yake California, Los Angeles, Marekani, amekuwa gumzo kwa miaka kadhaa tangu alipokubali kwa hiari yake mwenyewe kupigwa picha za utupu na kujiingizia mamilioni.
Ida ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 29, alizaliwa na mama Mtanzania na baba Mswidishi Septemba 27, 1981.
Alitisha mwaka 2008 alipofanikiwa kushinda kupiga pozi akiwa mtupu kwenye jarida maarufu la Playboy.

WANAFUNZI WALIOFANYA MAANDAMANO CHUO KIKUU(UDSM),KUFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO JUMATATU! 0 comments

13 november 2011
Wanafunzi takribani arobaini wa chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM),waliokamatwa siku ya ijumaa tarehe 11 mwezi novemba,kwa kufanya maandamano kuishinikiza serikari kuwapa mikopo wanafunzi wenzao wa mwaka wa kwanza,wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho jumatatu tarehe 14,kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kamanda wa polisi wa Kinondoni amesema kuwa wanafunzi hao watafikishwa mahakamani kujibu baadhi ya mashitaka ikiwemo kufanya maandamano bila kibari.Kesho uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) unatarajia kukutana na baadhi ya wadau wa elimu ya juu ikiwemo Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi,Serikari ya wanafunzi chuoni hapo,bodi ya mikopo ya elimu ya juu na Tume ya vyuo vikuu(TCU) ili kujadiri mustakabali wa masuala hayo ya mikopo,kuna tetesi  ya maandamano mengine kufanyika chuoni hapo endapo mambo hayo hayatapewa busara inayopaswa katika kuyashughulikia.

MBEYA FULL MABOMU,HOFU NA TAHARUKI VYATAWALA 0 comments

Jiji la MBEYA limechafuka,inasemekana hii ni kutokana na mkuu wa mkoa Abas Kandoro kuja na sera ya safisha jiji .
Tangu wiki mbili zilizopita alianzisha kampeni hiyo na badae akawahaidi kua atawaruhusu alhamisi lakin jana hakutekeleza ahadi yake hiyo hivo wafanyabiashara wakapanga kuanzisha fujo siku ya leo..

 Baadhi ya matukio katika jiji la mbeya leo,polisi na mabomu,mbwa n.k,raia wakiuguzwa hospitali,so ful taharuki


Habari zaidi inadaiwa barabara zimefungwa,maduka na biashara zote zimefungwa,inadaiwa gari moja limechomwa na mgambo mmoja ameuwawa na baadhi ya polisi wameumia,wanaume wapo mbele wameshika mawe huku wanawake wapo walikua nyuma wameshika ndoo kwa ajili ya kuzuia mabomu ya machozi kwa habari zaidi usichoke kunitembelea hapa!"soma habari yaliyotokea nako Chuo kikuu cha Daressallam(UDSM) hapa chini ya habari hii"

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KWACHAFUKA,MABOMU YARINDIMA,KISA MIKOPO YA ELIMU YA JUU. 0 comments

BREAKING NEWZ
Tayari mambo yamechafuka katika chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM)kwa kile kinachodaiwa ni kutopatiwa mikopo wanafunzi wa mwaka wa kwanza au kwa jina maarufu walilopewa la"no loan",hekaheka hizo zilianza tokea jana jioni tarehe 10 november,ambapo kikundi cha wanafunzi kadhaa katika hostel kuu za chuo hicho za MABIBO HOSTEL walionekana kuandaa maandamano hayo hii leo,polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wanafunzi hao huku hali ya taharuki na hofu ikijaa miongoni mwa baadhi ya wanafunzi hao na wafanyakazi wengine,hali hiyo imesababisha baadhi ya wanfunzi kutoingia darasani,kwa hofu ya baadhi ya wanafunzi wenzao kuwashinikiza wajiunge ktk maandamano hayo,mpaka ninaenda mitamboni magari ya polisi yaliyojaa vijana wa mwema yamejaa ktk Chuo hicho,kwa habari zaidi tazidi kukujuza so usichoke kunitembelea hapa..............!!
Hayo ndio mambo ya maandamano UDSM kama kawaida uzoefu unaonyesha waathirika wakubwa wa mambo kama haya huwa ni babiez(wanawake)

DR SLAA TUNDU LISSU NA WAFUASI WENGINE WA CHADEMA WAKAMATWA NA POLISI ARUSHA 0 comments

BREAKING NEWZKatibu mkuu wa CHADEMA, Wilbrod Slaa na mkurugenzi wa sheria wa chama hicho Tundu Lissu na wafuasi wengine kumi wa chama hicho wanafikishwa mahakamani muda mfupi ujao jijini Arusha.


kuna hatihati ya kutopewa dhamana maana vurugu zinaendelea kwani vijana wa chama hicho wanavunja vioo vya magari na muda mfupi uliopita wamefanya hivyo katika mitaa ya Sabena iliyoko karibu na stand kuu ya Arusha ,wanahojiwa na polisi kwa kuendesha mkutano jana. Cha ajabu jeshi la polisi lilikuwepo wakati wa mkutano kutoa ulinzi.kuwa nami tazidi kukuapdate!

TUNDU LISSU SHUJAA ALIYETOA WAFUNGWA 366 JELA NDANI YA MIEZI MINNE TU 0 comments

Aelezea siri yake na CHADEMA ilipoanzia
Mwanaharakati aliekuwa mbishi toka primary mpaka Chuo kikuu cha Dares salaam(UDSM)Yafuatayo ni mazungumzo kati ya mbunge machachari kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Tundu Lissu ambaye pia ni wakili wa kujitegemea
Mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo:


mgodi unaotembea: Tuanze na historia yako kwa muhtasari.


Lissu: Niliishi maisha ya furaha sana ya utoto. Tangu nikiwa shule ya msingi ni kama vile nilikuwa mwanaharakati.


Unajua shuleni kuna shughuli nyingi sana kama kuchota maji kwa ajili ya walimu, kulima mashamba ya walimu na kupanda.


Nilikuwa nikiona haya mambo hayako sawa, lakini pia kuna suala la kuwahi shuleni.


Sikumbuki kwa miaka saba ya shule ya msingi, kama kuna siku nimewahi zile namba. Siku zote nilikuwa mchelewaji na nimechapwa kweli.
mgodi unaotembea: Ni ukaidi wa makusudi?


Lissu: Siwezi kusema ni makusudi, lakini tatizo ni kuamka alfajiri saa 11 ili saa 12 niwe shuleni. Kwa hilo nilikuwa rebel (muasi).


Pia sikumbuki mahali ambako sikuwahi kubishana na walimu iwe primary school, secondary school, iwe chuo kikuu, siku zote imekuwa hivyo.
Lakini vile vile nilizaliwa katika familia ambayo mijadala ya kisiasa ilikuwa sehemu yetu. Baba yangu alisoma hadi darasa la sita, mama yangu hakusoma kabisa.


Kila jioni tunasikiliza kwanza taarifa ya habari na idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani; baada ya hapo ni mjadala mpaka saa tano au sita, mjadala wa kisiasa kuhusu mwenendo wa mambo duniani. Nilikuwa mtoto mdogo sana, lakini nilikuwa na ufahamu.Nafikiri nilikuwa miaka sita au saba hivi.
Wakati nikiwa darasa la kwanza (1976), nilikuwa nafahamu karibu viongozi wote duniani na miji mikuu mashuhuri.
mgodi unaotembea: Kutokana na ufahamu huo, ni viongozi gani hapa nchini walikuvutia wakati huo?


Lissu: Ni swali gumu kidogo. Si rahisi sana kusema nilivutiwa na Mwalimu Nyerere. Ukweli ni kwamba hapana, alikuwa sehemu ya mazungumzo ya kisiasa nchini. Siwezi nikasema nilivutiwa sana na Mwalimu.
mgodi unaotembea: Unaposikia jina la Julius Nyerere kwa sasa, unakumbuka nini?


Lissu: Ni hotuba za Mwalimu Nyerere kuhusu vita dhidi ya Uganda. Wakati huo nikiwa darasa la tatu mwaka 1978, nchi iko vitani tulichangishwa (familia) ng’ombe.


Baba yangu alitoa ng’ombe watatu kama sikosei ili kusaidia vita mpakani. Shuleni tuliimbishwa sana nyimbo kwamba Iddi Amini ni nyoka; ingawa baadaye nimekuja kugundua kwamba inawezekana kuna vitu vingine vingi hatukuambiwa kuhusu mgogoro wetu na Uganda.


Nakumbuka pia wakati huo tukiwa wadogo tulichimbishwa mahandaki. Nilikuwa na miaka 10, nilishangaa tunachimba (mahandaki) nje ya nyumba yetu halafu siyo marefu sana.


Lakini kuna kitu kingine kilichotafsiri mtazamo wangu kuhusu serikali ambao sio chanya sana. Nilipokuwa miaka kama sita hivi, nyumba yetu na wanavijiji wengine zilibomolewa halafu tukaachwa tu. Kina mama wanalia, kila mtu analia; halafu hawa watu wakavunja nyumba wakaondoka.
mgodi unaotembea: Hao wavunjaji walitumwa na nani?


Lissu: Unajua ukiwa na miaka 10 huulizi sana. Ni tukio ambalo haliwezi kuondoka katika kumbukumbu zangu kwamba; serikali inaweza kufanya vitu visivyo na akili (mantiki).


Sisi na wanakijiji wengine tumejenga nyumba, ingawa pengine hazikuwa nzuri sana wao (serikali) wametubomolea kwa jina la Operesheni Vijiji.


Baba yangu alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji wakati huo, baadaye (watendaji wa serikali) wakaja na kamba za katani na wataalamu ili kupima namna ya kujenga nyumba za kisasa, wanaita maendeleo.


Kwa hiyo, wazee wanatembea na kamba ya katani wanapima namna ya kujenga nyumba za kisasa , zijengwe kwa mstari ulionyooka. Lakini hatimaye hawakutujengea wala kutusaidia chochote.


Hali hiyo ilinifanya niamini kwamba pengine serikali haina watu wenye akili sana kama nilivyokuwa nikifirikia mwanzoni.
mgodi unaotembea: Ukiwa katika umri wa utoto, unakumbuka nini enzi za nchi kufunga mikanda na baa la njaa lililowahi kutokea?


Lissu: Kuna njaa ya mwaka 1974 serikali ilileta chakula kudhibiti njaa hiyo, nakumbuka kuna kitu (chakula) kinaitwa burga ilikuwa sijaanza shule baadaye tukaletewa ugali wa muhogo. Sisi kwetu tunakula muhogo wa kuchemsha. Ilikuwa hali tofauti.
mgodi unaotembea: Tueleze safari yako kielimu, ilikuwaje...ngumu au nyepesi tu.


Lissu: Wakati wa Operesheni Vijiji ilitokea mvutano wa kuhama. Baba yangu pamoja na wazee wengine walisafiri kutoka kijijini Singida wakaja Dar es Salaam kulalamika.


Walilalamika kwamba tunatakiwa tuhame kwenye kijiji chenye mashamba makubwa. Wakaja kupiga kelele na serikali wakati huo iliwasilikiza.


Lakini ikaibuliwa hoja kwamba; tuhame (kijiji) kwa sababu hakuna shule. Wakati ule, hoja ya vijiji vya ujamaa ililazimisha kuwapo huduma za kijamii.


Sasa ili kukabili hoja hiyo na tusiweze kuhamishwa, kuna mzee mmoja alijenga nyumba yake mpya, akasema sitahamia ili iwe shule ya watoto. Kwa hiyo, tukaanza shule lakini shida walimu.


Mmoja wa wadogo zake baba yangu wakati huo alikuwa amemaliza darasa la saba, hana pa kwenda, wakasema atakuwa mwalimu. Kuna mama mwingine mjanja mjanja kijijini, naye wakamwambia atakuwa mwalimu.


Kwa hiyo, tukaanza darasa la kwanza Aprili 5, 1976. Shule za miaka ile zilikuwa zinaanza Januari, lakini ya kwetu tulianza Aprili, kwenye nyumba ya tembe sio ya bati, na walimu wasio na mafunzo yoyote.


Hatukuwa na vitabu, swali likawa tutaandikia nini? Wazee wakachanga hela wakamtuma mtu Dar es Salaam aende kumtafuta mtu anaitwa Abdallah Nungu, amueleze tatizo la vitabu shuleni.


Kwa hiyo, tukamsuburi kwa wiki mbili huyu bwana alete vitabu. Akarudi na boski kubwa la vitabu na vile vibao vya kuandikia, ingawa awali tulikuwa tukiandika chini (ardhini). Hivyo ndivyo tulivyoanza shule wengine.


Lakini hilo lilikuwa darasa la kwanza kwenye hiyo nyumba ya mzee. Tatizo likajitokeza ni darasa la pili litakaa wapi, kwa sababu ilibidi darasa la kwanza wengine waanze.


Nyumbani kwetu baba alijenga nyumba jirani na mdogo wake, lakini huyo mdogo wake hakuwa akiishi hapo kijijini alikuwa Moshi, nyumba yake haikuwa ikikaliwa.


Mzee akasema darasa la pili hilo hapo (nyumba ya mdogo wake). Kwa hiyo, darasa la pili tukahamia kwetu (nyumbani). Natoka mlango huu, naingia mlango wa pili niko darasani. Baada ya hapo, tukaanza ujenzi wa shule ambayo ikaitwa Shule ya Msingi Mahambe.
mgodi unaotembea: Serikali haikutoa mchango wowote katika hatua za awali za ujenzi?


Lissu: Hatukusaidiwa na serikali katika ujenzi. Ilikuwa asubuhi tunakwenda shule, saa nane tunaporudi (shule) tunabeba vibuyu na ndoo za maji pamoja na mama zetu kupeleka eneo la kufyatulia matofali; shughuli iliyokuwa ikifanywa na baba zetu.


Mwaka mzima tumefyatua matofali na baadaye kuanza ujenzi. Kule kwetu kuna Wakatoliki wengi, pale eneo la ujenzi (wa shule) kulikuwa na padre anapita kwenda kusalisha kijiji cha jirani kila Jumatano. Kila akipita anakuta ujenzi unaendelea na watoto wanasaidia.


Huyo padre anaitwa Charles ni mu-Irish, kila siku anapita pale anakuta watoto na wazazi wanafanya kazi, nadhani alikuwa akijiuliza kuna nini? Siku hiyo akasimama. Alikuwa anatumia pikipiki kubwa....sijui ni kubwa (pikipiki) kweli au mimi ndiye nilikuwa mtoto na kuiona kubwa.


Akauliza, akaambiwa tunajenga shule. Akauliza serikali iko wapi? Akaahidi tukishamaliza ujenzi, ataleta mafundi kukamilisha kwa kuweka bati, ikaitwa Shule ya Wazazi.


Darasa la tatu tukaingia sasa kwenye darasa zuri na bora. Kuanzia hapo, kila mwaka nilipokaa pale shule ya msingi tulikuwa tunajenga darasa moja moja, hadi tulipomaliza mwaka 1979 tunaingia darasa la tano ndiyo kwa mara ya kwanza ikaitwa Shule ya Msingi Mahambe, na tutakaletewa mwalimu wa serikali.


Kwa hiyo, kati ya vyuo vikuu vyangu, chuo kikuu cha kwanza ni hicho....miaka minne ya kufundishwa na walimu wasio na mafunzo yoyote.
Siku hizi nikipita nikiwaambia watu shule niliyosomea na walimu walionifundisha, hawaamini.


Tulifundishwa na wanakijiji kabisa wasio na mafunzo! Serikali ilipoanzisha mpango wa UPE wale walimu walijiendeleza, wakaenda vyuoni na wapo ambao wamekuwa waalimu wanataaluma.
mgodi unaotembea: Hayo ni ya shule ya msingi, tueleze ya sekondari, unakumbuka nini hasa?


Lissu: Cha kwanza nimetoka nje ya kwetu (Singida), nimeenda kusomea Ilboru Sekondari, Arusha. Pale (Ilboru) maisha yalikuwa mazuri na nilikuwa mdogo kuliko wengine wote (wanafunzi). Sikuwahi kuwa kiongozi shuleni, na sikutaka uongozi. Viongozi wakati ule tuliwaita manyoka kwa sababu wanapeleka habari kwa walimu.
Lakini baadaye nilipoingia kidato cha tano na sita, Galanos Sekondari (Tanga), nilipewa uenyekiti wa Kamati ya Taaluma, lakini baada ya miezi sita hivi nikagombana vibaya sana na mwalimu wa taaluma, ikabidi nivuliwe madaraka.
mgodi unaotembea: Mlitofautiana katika jambo gani na mwalimu wa taaluma?


Lissu: Ni msimamo tu. Ilitokea kwamba mwaka 1988 niko kidato cha sita, sasa kidato cha nne na cha sita kila mwaka hufanya graduation (mahafali). Wakati huo, hasa Galanos na shule nyingi za sekondari, disko hazikuwa nyingi (mara kwa mara) kama sasa.


Kipindi cha kwenda kucheza disko ilikuwa wakati wa graduation. Sasa walimu wakaamua watoto wa kidato cha nne hawatakwenda kucheza disko. Mimi niko kidato cha sita, sasa tulipanga kwenda disko Korogwe Girls. Wakaamua (walimu) kidato cha nne hawatakwenda Korogwe Girls, badala yake waletewe taarabu.


Sikukubaliana, nikaandika makala inahoji uamuzi huo. Title yake naikumbuka hadi leo, inasema; “taarab for who’s benefit?” - taarabu kwa faida ya nani?


Halafu tukafanya mpango (wanafunzi) ikabandikwa kwenye mbao za matangazo shuleni, sikuandika jina langu halisi. Walimu wakauliza, wakapeleleza nani anaweza kuandika vitu kama hivi?.....wakanikamata.


Nikatuhumiwa kuleta uchochezi, nikasimamishwa shule, baadaye walinirudisha. Lakini kwa ujumla miaka ya sekondari ilikuwa mizuri, hapakuwa na njaa kama wakati huu.


mgodi unaotembea: Baada ya kuhitimu kidato cha sita, nini kilichofuatia?


Lissu: Nikaenda JKT Mbeya, kwanza nilipelekwa Mafinga, lakini sikukaa tukapelekwa Mbeya operesheni yangu inaitwa; Operesheni ya Programu ya Chama, mwaka 1989.
mgodi unaotembea: Unakumbuka nini kuhusu enzi za JKT?


Lissu: Ninachokumbuka mjadala wa vyama vingi ulikuwa umeiva na CCM hawataki vyama vingi. Ilikuwa mwaka 1989/1990, kwa Katiba ya CCM wakati huo, kulikuwa kuna mkoa unaitwa Mkoa wa Majeshi, ulikuwa mkoa sawa na mingine katika chama.


Kwa hiyo, wakatuma wajumbe wao wa Mkoa wa Majeshi kutembelea kambi zote za jeshi na JKT Tanzania nzima, kueleza msimamo wa CCM. Waliokuja Itende JKT kwetu nawakumbuka ni Omari Mahita wakati huo ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Kanali Andrew Shija na mtu mwingine simkumbuki.


Nawakumbuka Kanali Shija na Omari Mahita kwa sababu walijenga hoja kwamba haya mageuzi (vyama vingi) hayatuhusu kwa hiyo tusishabikie yasiyotuhusu; eti yanayowahusu Wazungu, Ulaya Mashariki na kwingine.


Nakumbuka nilipambana vibaya sana na Omari Mahita kwenye huo mkutano. Nilisimama kuuliza maswali nikitambua kuwa kabla hawajaja, Mwalimu Nyerere alihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Vijana wa CCM, Mwanza na akasema wanaodhani mageuzi ya Ulaya Mashariki hayatuhusu, ni wajinga.


Kwa hiyo, nikamuuliza RPC Omari Mahita nikamwambia kwamba Mwalimu Nyerere alisema wanaofikiri mageuzi ya Ulaya Mashariki hayatuhusu ni wajinga, na wewe umekuja na timu yako unatuambia haya mambo ni ya Wazungu hayatuhusu.


Sasa mjinga ni Mwalimu Nyerere aliyesema yanatuhusu au nyie ambao mnatuambia kwamba hayatuhusu?
mgodi unaotembea: Bila shaka ulitumbukia katika uhasama wa ghafla na meza kuu. Hali ilikuwaje?


Lissu: Omari Mahita ni mweupe sana, basi, ghafla akabadilika rangi akawa mwekundu. Ikawa makamanda kadhaa wakasimama tayari kumshughulikia huyu serviceman...maana nilishapita ukuruta. Wakasimama kutaka kumshughulikia anayetukana maofisa wa jeshi.


Lakini kanali Shija (marehemu sasa) akasimama akanitetea. Akasema; hoja ya serviceman ni sahihi kabisa, Mwalimu ndivyo alivyosema. Kwa hiyo, hatuwezi....kusema hayatuhusu. Maana yake tayari nilianza kusakamwa pale... akasema ni kweli hatuwezi kukwepa haya mawimbi na upepo. Shija akapiga siasa, na hatimaye akaniepushia kibano.
mgodi unaotembea: Kwa hiyo makamanda wenyewe kwa wenyewe walitofautiana mbele yenu?


Lissu: Walitofautiana na baada ya hapo, hakuna ofisa wa JKT aliyenigusa tena. Wengi baada ya hapo wakaamini mimi ni usalama wa taifa. Maisha yakawa mazuri. Hakuna aliyenigusa kwa sababu kama nimezungumza vile na kanali wa jeshi, kwa sababu mkuu wa kambi mwenyewe hakuwa kanali, alikuwa luteni kanali, sasa mimi nimetetewa na Kanali Shija.


Kwa hiyo nilikuwa nakula shushi (mambo mteremko).


Baada ya hapo nikaenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Miaka ile ulikuwa huendi chuo kikuu kama si mwanachama wa CCM na sehemu ya mafunzo unayopata JKT ni pamoja na itikadi ya CCM na mnapomaliza mafunzo mnakabidhiwa pia kadi za chama. Kwa hiyo, nilikuwa mwanachama wa CCM na hiyo ni muhimu watu wakafahamu.


Lakini nilikuwa mwanachama kwa sababu tu nilitaka kusoma. Ndivyo maisha yalivyokuwa na baada ya hapo. Nilipoingia chuoni kadi haikuwa na kazi sana kwangu. Siku ya kwanza chuo kikuu hadi naondoka, mijadala yote nilikuwa mstari wa mbele kabisa pamoja na kwamba sikuwahi kuwa kiongozi.
mgodi unaotembea: Katika mijadala yenu chuoni hasa ile mikubwa, hoja gani unakumbuka zilitikisa uongozi au hata nchi?


Lissu: Wakati huo, dunia na nchi ilikuwa ikibadilika, hatukuwa tayari tena kutawaliwa na mfumo wa chama kimoja, eti usipokuwa na kadi ya chama huendi chuo. Nikiwa mwanafunzi, uchangiaji wa gharama za shule ulianza wakati huo.


Nilikaa mwaka mzima nyumbani kabla ya kuingia chuo kikuu kwa sababu mwaka 1989 wanafunzi wa UDSM waligoma, chuo kikafungwa.


Pamoja na kwamba sikuwa sehemu ya huo mgomo wakati huo nilikuwa JKT, lakini madhara ya mgomo yalinigusa kwa kukaa nyumbani mwaka mzima. Nilipojiunga chuo mwaka 1991, tayari vuguvugu lilikuwa kubwa sana. Na upinzani dhidi ya uchangiaji gharama za elimu ulikuwa mkubwa sana.
mgodi unaotembea: Mliguswa vipi na tukio la kumdhalilisha Rais Mwinyi wakati ule chuoni UDSM?


Lissu: Chuo kilifungwa kutokana na tatizo hilo mwaka 1989. Ni tukio lililotugharimu ambao ndiyo tulitaraji kwenda kuanza masomo. Tulikaa nyumbani mwaka mzima.
mgodi unaotembea: Katika changamoto za mageuzi chuoni, baadaye ulijiunga na chama gani baada ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa?


Lissu: Kama nilivyosema, nimezaliwa rebel , na hivyo haikuwa ajabu hata kidogo mimi kujiunga na chama cha upinzani ambacho kilivutia wasomi - NCCR-Mageuzi. Ilikuwa ni hatua inayotegemewa.


Nisingeweza kuwa CCM au CHADEMA kwa sababu kilikuwa chama kisichokuwa na msimamo mkali....hawa watu ni waoga, wanaogopa kuweka msimamo mkali. Ni kama chama cha kibepari hivi na mimi kimsimamo nimekuwa Mjamaa wa mrengo wa kushoto kabisa.
mgodi unaotembea: Uchaguzi wa kwanza baada kuruhusiwa vyama vingi mwaka 1992 ulifanyika 1995. Ulishiriki vipi uchaguzi huo?


Lissu: Ingawa jimboni kwetu (Singida Kusini wakati huo) mwanzo hapakuwa na uchaguzi wa vyama vingi, lakini ilikuwa sehemu ya changamoto kisiasa, hata wabunge waliokuwa wakichaguliwa walidumu kwa muhula mmoja tu.


Sasa ghafla tukawa na demokrasia pana zaidi - vyama vingi, lakini kwenye uchaguzi huo (1995) ikaelekea CCM itapita bila kupingwa. Kwa hiyo nikajitokeza kugombea ubunge jimbo la Singida Kusini.


Lakini wakati naanza mchakato wa kuwa mgombea, nikapata scholarship ya Serikali ya Uingereza kwenda kusoma Master’s (Uzamili). Nikaenda shule kuripoti, nikawaambia narudi nyumbani kujaribu ubunge, nikishindwa nitarudi.


Nikatoka Uingereza kuja kugombea ubunge mwaka 1995, nikiwa na miaka 27. Nikarudi shule baada ya kushindwa. Safari yangu ya kisiasa ilianza kujitokeza kipindi hicho.
Nikamaliza shule yangu mwaka 1997, nikaoa na nikahamia Dar es Salaam (kutoka Arusha alikokuwa akifanya kazi kama mwanasheria ofisi binafsi).
mgodi unaotembea: Katika harakati zako, tukio gani kubwa unakumbuka lilikutia msukosuko au kuibua katika jamii?


Lissu: Tukio la kwanza kubwa ilikuwa ni mradi wa ufugaji kamba delta ya Rufiji. Mradi wa Mzungu mmoja wa Ireland anaitwa Reginald Nolan.


Alipewa na Serikali ya Mkapa hekta 20,000 ili atengeneze mabwawa ya kufuga kamba kwenye delta ya Rufiji katika maeneo ambayo yana vijiji karibu vinane, watu walima na kuishi, kuna msitu ya mikoko pale. Yote ile Reginald Nolan akapewa ili atengeneze mabwawa. Sisi kama watetezi wa mazingira kupitia Chama Cha Wanasheria wa Mazingira – LEAT, tulishikia sana bango mradi wa Rufiji.


Tulifanya kazi kubwa. Niliratibu kampeni ya kimataifa kwa kila njia, ikiwamo mitandao ya kimataifa ya wanaharakati kuupinga mradi huo.


Hatimaye, Benki ya Vitega Uchumi ya Ulaya (European Investment Bank) iliyokuwa itoe mkopo kwa Nolan ambao ungedhaminiwa na Serikali ya Tanzania, wakasema hawatatoa mkopo na kwa hiyo, mradi mzima ukasambaratika.


Niliwahi kushiriki mdahalo kwenye kituo cha televisheni nchini kuhusu mradi huo wa kamba, nikiwa mimi, mmiliki wa mradi na mwandishi wa habari wa siku nyingi, James Mpinga. Kwa mara ya kwanza ndipo nilipoanza kuonekana kwenye televisheni katika kipindi cha Hamza Kasongo Hour, Oktoba 1998.


Tuliwasambaratisha kila mahali. Tukapata nyaraka za Baraza la Mawaziri zilizosema mradi ni wa hovyo, lakini umepitishwa kinyemela.
mgodi unaotembea: Katika mchakato mzima wa harakati hizo, uliwahi kukumbwa na vitisho vya aina fulani?


Lissu: Vitisho vingi. Unaweza kufika ofisini ukakuta bahasha yenye ujumbe wa vitisho imepenyezwa chini ya mlango.


Baada ya hapo Machi, mwaka 1999, kuna kampuni moja wenye ginnery (kinu cha kuchambua pamba). Ni kampuni ya ki-Swisi. Wakaja ofisini kwetu (LEAT) wakaomba tuwafanyie utafiti juu ya madhara wanayoweza kupata kutokana na mgodi uliokuwa ukijengwa Geita.


Walitaka kubaini kama shughuli za mgodi zitaathiri shughuli zao za kusafisha pamba.


Kwa hiyo, nikapewa hiyo kazi. Nikasafiri kwenda Geita, asubuhi yake (baada ya safari) wenyeji wangu wakanipeleka wanakojenga mgodi.


Nikakuta vijiji vinabomolewa kwa magreda na mbele yake wametangulia askari wenye bunduki. Kijiji kile kilipitiwa na barabara, sasa upande wa pili wa barabara yuko Mkuu wa Wilaya, Halima Mamuya, OCD na maofisa wengi.


Mkuu wa Wilaya ya Geita ameshika kipaza sauti, anawaambia wanakijiji kwamba niliwaambia mlipwe fedha (fidia) mmekataa, sasa mtajua mtakwenda wapi.


Pale kwenye shimo kubwa lenye kina cha Kilomita kama tano wanakochimba dhahabu ndipo kilipokuwapo kijiji cha Mtakuja.


Nilishuhudia mgodi wa kwanza ukianzishwa kwa kuharibu kijiji ambako kulikuwa na makazi pamoja na mazao...mahindi yanayoelekea kukomaa, na wakati huo nchi ilikuwa imekumbwa njaa kwa sababu mwaka uliopita kulikuwa na mvua za el-nino.


Hali ile ilinikumbusha wakati wa operesheni vijiji ambako nyumba yetu na za wanavijiji pamoja na mashamba viliharibiwa. Nilishangaa serikali kuharibu mashamba ya chakula.


Nikaandika ripoti yangu, nikawapelekea wenye kinu cha pamba na kupendekeza kwamba tunahitaji ginnery kukaa na wananchi kijiji ili kupambana na uhalifu huo.


Nikawaambia nyie mna hela, wanakijiji watawapa ile human element, idadi ya watu ambao wanaathiriwa. Ukizungumza athari, ukaonyesha watu wanabomolewa ina value kubwa sana katika mapambano. Kwa hiyo, wanakijiji mkiwaacha wakasambaratishwa, hata nyinyi hamtabaki.


Wakaniambia sisi ni wawekezaji, nikawaambia wenzangu katika LEAT kwamba ugomvi mkubwa katika miaka inayokuja ni ugomvi wa madini.


Kwa hiyo, kutoka Geita kwenda Bulyanhulu ni mwendo wa dakika 45. Katika kuchunguza makampuni ya madini yanafanya nini kwa wananchi, kitu cha kwanza utakachokutana nacho ni Bulyanhulu. Ndio eneo ambalo kulitokea maafa makubwa zaidi.


Mwaka 1999 nikapata nafasi kwenda Marekani kuwa mtafiti katika taasisi ya World Resource Institute kwa miaka mitatu. Nikawaambia World Resorce Institute nitafanya kwa sharti moja; kwamba kazi niliyoanza kuifanya katika LEAT ya madini niendelee nayo.


Nikaondoka kwenda Marekani Septemba 1999 na kwa miaka mitatu yote mnayojajua juu ya Bulyanhulu yalipatikana katika kipindi hicho. Karibu kila mwezi nilirudi Tanzania kuendelea kutafiti suala hilo la Bulyanhulu.


Tulipata ushahidi wa picha za video na nyingine unaothibitisha kwamba watu wengi waliuawa. Hizo picha ni za jeshi la polisi na kampuni yenyewe.


Tulikuwa kila tunapopata video hizo tunazitangaza hadharani. Mwaka 2001 tulifanya press conference kubwa Maelezo kuthibitisha kwamba tunao ushahidi wa picha za video zinazothibitisha mauaji hayo kutokea.


Nilikuwa mimi na Rugemeleza Nshala. Baada ya mkutano huo, mimi nikaondoka kurudi Marekani. Lakini huko nyuma, baada ya tarehe 23, Polisi wakavamia ofisi zetu za LEAT na nyumbani kwangu wakitafuta huo ushahidi.


Na wakati huo Jeshi la Polisi likasema huyu mtu ametoroka, anatafutwa na Interpol, kwa hiyo akamatwe. Wenzangu baadaye walikamatwa.


Niliporudi Marekani walinikamata na kuniweka kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam. Nilipokuwa kituoni humo nilifanya ujanja nikaingia na simu na nikafanya mahojiano na magazeti ya Canada na Marekani usiku kucha. Kesho yake ilikuwa sikukuu ya Krismasi. Nikafuatwa na polisi, nikaambiwa napelekwa mahakamani.
mgodi unaotembea: Tueleze kujiunga kwako na CHADEMA, kulikuwaje?


Lissu: Kujiunga na CHADEMA mwaka 2004 sababu ilikuwa Tarime na suala la kampuni za madini. Harakati za madini Tarime nilizianza mwaka 2003.


Wakati ule mtu aliyenipokea Tarime ni marehemu Chacha Wangwe. Nilimkuta ana kesi 10 za jinai wakati huo akiwa diwani wa CHADEMA. Akaniambia; wanataka kunifunga hawa...nikamwambia hawawezi, wanakutisha tu.


Alisumbuliwa sana, na Tarime ilikuwa inatisha kama ilivyo leo. Mbowe akanipigia simu akaniomba nisaidie kisheria kumtetea Wangwe, chama kitagharimia usafiri. Kwa hiyo, nikaanza kazi ya kuwapa huduma ya kisheria na katika kipindi cha miezi minne nimetoa gerezani watu 366 waliokuwa wanatumikia vifungo.


Siku moja Mbowe akaniambia nitafute watu wengine wanataaluma ili wajiunge na CHADEMA. Nikamuuliza kwa nini unafikiria mimi ni mwanachama wa CHADEMA? Alikuwa miaka yote anafikiria mimi ni mwenzao, kumbe mimi ni NCCR-Mageuzi.


Akauliza kwa nini si mwanachama wa CHADEMA? Nikamwambia hujawahi kunipa sababu za kwa nini niwe mwanachama wa CHADEMA. Kama unataka niwe, niambie tu.


Kwa hiyo, hivyo ndivyo nilivyoingia CHADEMA. Kwa maisha yangu kwa historia yangu na msimamo wangu, mimi ni mwanahakarati, na pengine Rais Kikwete hakosei sana anaposema vyama vingine ni vya wanaharakati.


mgodi unaotembea: Unazungumziaje nafasi yenu Bungeni, hasa ikizingatiwa suala la idadi na ubora wenu?


Lissu: Bunge kama unaelewa sawawa linakupa nafasi ya kuibua mijadala. Siku zote sasa nimeelewa kwamba Bunge si mahali pazuri pa kutatulia migogoro, lakini ni mahali pazuri pa kuzungumzia na ku-mobilise nguvu ya umma. Hayo matatizo ya kisiasa au kikatiba, hayatatuliwi bungeni isipokuwa yanazungumzwa.


Suala la wingi, kwa maana ya idadi au ubora wa wabunge, bila kujali idadi lina umuhimu wake.


Kwa mfano; inapofika wakati wa kupitisha sheria au bajeti, hatuwezi ingawa tunao wabunge bora zaidi na wajenga hoja wazuri. Kwa hiyo, hapo ‘ujinga wa wengi’ ndipo unaposhinda.


Kama unaitumia nafasi hiyo bungeni vizuri, kama ambavyo tumekuwa tunafanya, hiyo itakuwa inatusaidia kujenga nguvu kubwa nje ya bunge. Inategemea unatumiaje hiyo fursa ya Bunge.
mgodi unaotembea: Ulikuwa Tarime hivi karibuni. Wako wanaohoji ulikwenda kutafuta nini wakati ni eneo lenye mbunge wake.


Lissu: Labda niwajibu hao wajinga wasiojua nilikuwa nafanya nini Tarime. Kwa historia yangu na Tarime, ilikuwa ni wazi ningeenda Tarime baada ya kutokea masuala haya (mauaji) na ndugu zao kukataa kuwazika hadi uchunguzi.


Ningekuwa sio mbunge pia ningekwenda Tarime. Nina historia ndefu ya mapambano ya kudai haki Tarime.


Yaliyotokea yanafamika - tulikamatwa na kuwekwa kwenye selo Tarime, tumeshtakiwa. Ni hali halisi ya Tarime. Ni eneo la vita, ni janga la kitaifa kama nilivyoeleza baada ya kuachiwa kutoka gerezani.
Tarime ya leo ni mbaya kuliko Tarime ya 2003 nilipokwenda kwa mara ya kwanza ambapo mamia ya watu wa Nyamongo walikuwa gerezani. Tarime ya leo ni ya mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi. tangu tuwashinde (CCM) uchaguzi. Mauaji ya kwanza Tarime yalifanyika Julai 20, 2005.


Hadi kuua hawa wa juzi watano, sasa wamefikia watu 28 waliouawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe.
mgodi unaotembea: Lakini kiini cha tatizo nini? Je, ni mwekezaji au jeshi la polisi?


Lissu: Tatizo ni mwekezaji, polisi na Serikali ya Tanzania. Kusingekuwapo mwekezaji, watu wasingeuawa.
mgodi unaotembea: Lakini kama tatizo ni pamoja na polisi au serikali kuna migodi mingine mauaji hayaendelei kama Tarime?


Lissu: Katika sekta ya madini unakuja na umwagaji damu. Bulyanhulu, Tarime, Geita, Nzega hakuna mahali ambapo wawekezaji wameweka mgodi wa dhahabu wa kisasa bila kuangamiza uchumi wa wenyeji, bila kuwaondoa kwa mabavu ya kijeshi.
mgodi unaotembea: Kifanyike nini?


Lissu: Ni mambo mawili ya kuchagua. Kwanza, je, tunataka huyo anayeitwa mwekezaji achume mali na inunuliwe kwa damu za Watanzania? Inunuliwe kwa Watanzania kukosa haki na kwa uchumi wa Watanzania kusambaratishwa?


Au tuamue kwamba maisha ya Watanzania ni bora zaidi kuliko dhahabu.
Kwa maoni yangu, haiwezi bei ya dhahabu ikawa sawa na maisha ya mtu mmoja. Watanzania wameshauwa kwa risasi na kwa kunywa maji ya sumu yanayotokana na mwekezaji.


Tarime imejaa vijana wanaoshitakiwa kwa kesi za ugomvi na mgodi, lakini sasa hivi wanashtakiwa kwa kesi za mauaji au uhalifu wa kutumia silaha!


Wakati nakwenda Tarime kwa mara ya kwanza, kesi zilizokuwa zikifunga watu zilikuwa uchochezi na kuvamia eneo la mgodi, lakini leo kesi za Tarime ni mauaji.


Hata ukikamatwa kwa kurushwa jiwe ambalo halijampiga mtu yeyote, utashtakiwa kwa mauaji au uhalifu wa kutumia silaha!


Na unashtakiwa kwa hayo makosa mawili kwa sababu huwezi kupewa dhamana. Kwa hiyo, polisi wasipofanya upelelezi utafia gerezani.


Nilikamatwa Tarime nikakaa gerezani. Naweza kuthibitisha kuwa Tarime kuna watu zaidi ya 400 wanaokabiliwa na kesi za mauaji.
Sasa njoo huku ambako hakuna mgodi, leo biashara ya teksi Tarime mjini ni biashara ya mapolisi kwa sababu wafanyabiashara wa kawaida pale mjini aidha wako gerezani wakikabiliwa kwa mauji au wengine wameuawa.


Selo niliyofungwa mimi Tarime inatumika kwa kitu kimoja tu, nimeambiwa kuna watu wengi sana wameuawa, wameumizwa sana. Kuna mtu mmoja amepigwa risasi tano miguuni kwenye kituo cha polisi na mkononi amepigwa risasi mbili, na mkono umekatwa.


Kuna mtoto wa miaka 12 selo niliyolala mimi. Bunge hili limepitisha sheria mwaka juzi, sheria ya mtoto inayosema mtoto wa miaka 18 hawezi kupata adhabu ya kifungo.


Huyu mtoto ana miaka 12 anakaa kwenye gereza na wafungwa watu wazima waliopatikana na hatia. Napeleka hoja binafsi bungeni kuomba iundwe kamati teule ya Bunge kuchunguza suala hili.
source-raiamwema

SAIKOLOJIA NA MAUMBILE 0 comments

AINA NA MAKUNDI YA WATU.


Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni


Introvant: watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina


hapa kuna makundi mawili
1.Melancolin 2. Fragmetic


2. extrovants: wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao
Hapa kuna makundi mawili
1. Sanguine 2. Colerick


Na sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao


1.MELANCOLIN
Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo
-wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligency Quetient)
-ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
-wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
-ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
-wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
-Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji --wanamaombi wazuri sana kiimani)
-Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
-Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
-Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
-Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasanu si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
-Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
-Wakata tamaa wanapokosolewa.
-Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
-Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
-Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo
-Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
-Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
-Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)
-Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
-Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana
-Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe
-Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
-Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
-Wana busara na hekima nyingi
-Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
-Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
-Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
-Ni kundi la watu wanoridhika haraka
-Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa
-Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
-Kundi linalopenda amani na utulivu
-Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
-Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu
-Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
-Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
-Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
-Wakati mwingine hupenda kujikataa.
-Ni waaminifu na wasema ukweli
-Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
-Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
-Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
-Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
-kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tama mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani]
-Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
-Kwa upamnde wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua
Mifano ya watu wa kundi hili: Musa (wa biblia) Yesu Kristo, Bob Marley, Celin Dion
2: FLAGMETIC
-Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
-Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini
-Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalili shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia)
-Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
-Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao
-Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea
-Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
-Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili
-Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hatawaliwa na mifano na takwimu halisia
-Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu)
-Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili
-Ni watu wasioumizwa kufanya makosa
-Hawapendi kuwaamini wenzao
-Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali
-Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
-Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao)
-Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
-Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka)
-Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea
-Si watu wanaojali muda na ratiba
-Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
-Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani
-Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
-Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)
-Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani
-Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu)
-Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko
-Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
-Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
-Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote
-Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao.
-Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia
-Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.
3.SANGUINE
-Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo)
-Ni wacheshi sana
-Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea
-Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza
-Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine
-Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili
-Wanapenda sana kujisifu na kujikweza
-Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia
-Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
-Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa uhakika
-Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
-Muda wote wako nadhifu (ni wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu)
-Wana kiherehere sana.
-Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau
-Ni vinyonga katika tabia zao (wanuwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua wasiwagundue kirahisi)
-Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi kuyaacha
-Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi
-Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja: __inasemekana kutokana na maneno yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.)
-Wawapo kwenye jamii hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao.
-Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha
-Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi
-Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama za kuhubiri kwa mvuto na ushawishi wa pekee)
-Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo
-Ni kundi la watu waoga sana (wanajiamini sana kwa maneno lakini kivitendo ni kunguru)
-Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji)
-Wanapenda kujaribu kila jambo linalokuja mbele yao
-Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
-Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine
-Hawana aibu hata mbele ya watu wasiowafahamu wala kuwazoea
-Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
-Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama madini)
-Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi)
-Ni watu wa mipango isiyoona mbali (wakurupukaji) (Ministers of emmergency affairs)
-Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kirahisi na kwa dhati)
-Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
-Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
Mfano ni Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kiti (alipomwona Yesu anatembea juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu (aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri (aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa (alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa)


COLERICK


-Wana uwezo wa kawaida kiakili
-Ni wa wakali na wakaidi
-Hawana huruma wala unyenyekevu
-Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
-Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
-Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa
-Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
-Watu wasiokata tamaa mapema
-Wanajiamini kupita kiasi
-Hawana uoga ni majasiri sana
-Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
-Kundi la watu wenye nguvu nyingi
-Ni madikteta
-Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
-Watu wa kulipiza visasi
-Watu wa vitendo kuliko maneno
-Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
-Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
-Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
-Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo -wa kiukandamizaji
-Hawajui kubembeleza
-Hawaongei wala kucheka ovyo
-Wanapotenda jambo huwa wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya kurudishiwa hicho alichokitoa
-Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa hasara
-Si watu wanaopenda suluhu na amani
-Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
-Hawapendi starehe kwa wingi
-Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki na shida
-Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
-Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha
-Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd Amin, Hitler, etc


*SI TABIA ZOTE ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA


MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU
-Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani
-Huwezi kujibadilisha kundi
-Kujifahamu kundi lako kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kuwa makini namna ya kuishi nao
-Inawezekana kabisa kujifahamu upo kundi gani na pia kwa kusoma na kutazama ni rahisi kutambua makundi ya wengine


*NITATAMBUAJE MIMI NI WA KUNDI GANI?
-Watu wengi wana tabia za makundi zaidi ya moja
-Kwa wale tabia zaidi ya asilimia themenini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure (i.e pure sanguine etc)
-Kama una tabia kutoka kundi zaidi ya moja, unaunganisha majina ya makundi mawili yenye tabia nyingi zaidi, unaanza jina la lile lenye asilimia nyingi zaidi
*Mfano: flag-coleick; cole-flagmetic, flag-colerick , sangu-melancolic, melanco-sanguine: etc
Unaweza kuwasiliana nami kupitia paulchengula@gmail.com na kwa facebook au just call 0755334530
source:Albert Sanga