Roma afunika tamasha Chuo Kikuu(UDSM) Linnah azomewa

Wasanii mbalimbali wamefanya show leo tarehe 24 october 2011,wakiwemo Roma Mkatoriki,Linnah,Barnaba na wengineo
Tamasha hilo lililoandaliwa na serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Daressalaam(UDSM)yaani DARUSO limefanyika katika Hostel za chuo hicho za MABIBO HOSTEL
Tamasha hilo limekuja ikiwa ni kuazimisha miaka hamsini ya Serikali ya wanafunzi ya chuo hicho,Tamasha hilo limedhaminiwa kwa ushirikiano na Utawala wa chuo hicho,huku tamsha hilo likipangwa kuhudhuriwa na kuzinduliwa na watu mbalimbali ikiwemo Waziri mkuu wa serikari ya wanafunzi ya zamani mbunge wa Kigoma kaskazini Mhe; Zitto Kabwe,wengine ni Mbunge wa Ubungo mhe:John Mnyika na wengineo,
Wanafunzi wala mpaka kusaza:
Katika Tamasha hilo,kuhusu suala zima la chakula na vinywaji ilikuwa ni free, so hii imesababisha guys kufurahia tamasha hilo coz lilikuwa full shangwe
Roma afunika Linnah azomewa na kushushwa jukwaani
Kama kawaida Tamasha hilo lilifana sana kwani Msanii anaekuja kasi katika muzik wa kizazi kipya Roma Mkatoliki amefunika katika tamasha hilo na kushangiliwa na wasomi hao,huku Msanii kutoka THT Linnah hakupewa support na wasomi hao,coz ilimlazimu kushuka jukwaani,hiyo ikitokea baada ya kelele na miguno huku baadhi ya wanafunzi hao wakithubutu kumrushia chupa za maji jukwaani,mara baada ya tukio hilo Linnah kiroho safi baada ya kuimba nyimbo kadhaa akaona bora ashuke jukwaani,ambapo ikafika zamu ya Barnaba ambae atleast alijaribu kushitua kidogo umati,huku baadhi ya wanafunzi wakisema "Linnah kilichomponza ni kubana sauti yake kwa nyodo na kile kivazi chake".
source:Nilikuwepo kwenye tukio

0 comments:

Post a Comment