WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAFA KWA AJALI

20 november 2011


(Moses Mwale (Zambian) mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyesalimika kati ya kumi, watatu wamelaza Hospitali ya Ngara.)


Ajali ya Basi la Taqwa na Lori la Azam iliyotokea jana Lusaunga wilaya ya Biharamulo imeteketeza wanafunzi 6 wa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa wakichukua Masters of Science in Mathematical Modelling, walikuwa wakienda Rwanda kwenye warsha ya Pure Mathematics.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Kozi hiyo yenye wanafunzi toka mataifa mbalimbali katika UDSM Dk Wilson Manera Charles alisema wanafunzi hao ni kati ya kumi ambao waliteuliwa kuwakilisha katika warsha hiyo ya wanahisabati inayofanyika kila mwaka, wannne wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu, aliongeza kuwa waliokufa ni Mzambia mmoja, Malawi 2, Mganda 1 na Watanzania 2.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya alisema vimeongezeka vifo 2 na kufikia jumla 18 na kuwa mpaka sasa maiti zote zimetambuliwa na nane kuchukuliwa na ndugu zao kwa maziko, mingine insaburi ndugu.
Pia aliongeza kuwa Mtoto mdogo wa kiumu anayekadiriwa kuwa na miaka miwili na nusu ambaye mama yake amefariki ajalini amehamishiwa hospitali ya Bugando Mwanza kwa matibabu zaidi.
Majeruhi walioko Biharamulo ni Tina Elisha, Rose Nula, Janet Kisanga, Moses Mwale, Joseph Bigilimana, Anicet Mrundi, Joseph Baltazary na Masalu Leonard.
Maiti zilizotambuliwa ni Abiba Juma, Faida Abdalah, Aziza Said, Andi Ibrahim, Chanda Congo, Nshaija Muganyizi na Kasimu Dadi, wengine ni Erick Eliude, Chinuka Hamajata na Ndizeye Pili.kwa habari kama hizi na nyingine nyingi usikose kutembelea blog hii!

0 comments:

Post a Comment