KONA YA SHERIA: HAKI ZA MTUHUMIWA MBELE YA POLISI1. Mtuhumiwa ni nani?
Ni mtu yeyote ambaye anawekwa chini ya ulinzi na
polisi au chombo cha usalama kwa kutuhumiwa
kufanya kosa la jinai.
2. Makosa ya jinai ni yapi?
Ni makosa ambayo mtu akipatikana na hatia hupe-
wa adhabu.
Ni makosa kama wizi, ubakaji, mauaji, kufanya
makosa ya kuhatarisha amani n.k.
3. Haki za Mtuhumiwa
(a) Mtuhumiwa anapowekwa chini ya ulinzi
ana haki ya kuelezwa sababu za kukamatwa
au kutiliwa mashaka.
(b) Mtuhumiwa ana haki ya kudai risiti ya orodha
ya vyombo/mali atakayokuwa nayo wakati
wa kumpekua zile zinazochukuliwa kituoni na
pale anapokabidhiwa polisi.
(c) Mtuhumiwa akiwa mwanamke lazima
kukaguliwa na polisi mwanamke.
(d) Mtuhumiwa ana haki ya kudai kibali cha
hakimu pale majadiliano/maelezo kwa polisi
yanapozidi saa nane.
(e) Mtuhumiwa anayo haki ya kudai awasiliane na
mtu anayemtaka akiwa chini ya ulinzi.
Kwa mfano rafiki, ndugu au wakili.
(f) Mtuhumiwa ana haki ya kufikishwa
mahakamani katika muda usiozidi masaa 24.
(g) Mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya wakati
wa mahojiano na polisi na anapaswa kuelezwa
kwamba chochote ambacho mtuhumiwa
atawaeleza polisi inaweza kutolewa
mahakamani kama ushahidi dhidi yake.
(h) Mtuhumiwa ana haki ya kutojibu maswali
ya polisi na kukaa kimya hadi polisi
anayemuuliza/endesha mahojiano awe
amemueleza mtuhumiwa yafuatayo:
(i) cheo alicho nacho na jina lake
(ii) mtahadharishwa kwamba yuko chini ya ulinzi.
(iii) kosa alilofanya au sababu ya kuwa chini ya ulinzi.
(iv) anayo haki ya kudai asomewe kilichoandikwa
kabla ya kuweka sahihi kwenye maelezo.
Mtuhumiwa anayo haki ya kupewa heshima na
kuthaminiwa kwamba ni binadamu. Hakuna ruhusa
kumtesa mtuhumiwa na kumdhalilisha anayo haki
ya kudai matibabu.
(i) Mtuhumiwa anaweza akaomba dhamana wakati
yuko chini ya ulinzi wa polisi.

Imeandaliwa na: Paul Chengula(mgodi unaotembea) 
Kwa maelezo zaidi juu ya tatizo la kisheria ulilo nalo au unahtaji sheria(ACT) yeyote ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,wasiliana nami kwa 0755334530 au paulchengula@gmail.com

0 comments:

Post a Comment