WALIOFUKUZWA CHUO KIKUU UDSM KUKATA RUFAA,CHADEMA NAYO YATOA TAMKO

17 novemba 2011
picha na maktaba yangu:wanafunzi UDSM wakiandamana
Baadhi ya wanafunzi waliofukuzwa UDSM wana mpango wa kukata rufaa kutokana na hukumu waliyopewa na uongozi wa chuo hicho,wakiongea na waandishi wa habari ikiwemo star tv wanafunzi hao wanasema watakata rufaa ili kuwezeshwa kuendelea na masomo chuoni hapo,baadhi ya wanafunzi hao wamesema utawala wa chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) haukuwatendea haki ya kikatiba ya kutokusikilizwa,wakiongea baadhi ya wanafunzi hao wamesema hawako tayari kuomba radhi kwani wanajua walichokuwa wanapigania kilikua ni cha kweli na cha msingi, wanafunzi hao wamefutiwa udahili ktk chuo kikuu cha Dar(UDSM) baada ya kufanya mgomo kwa madai ya kupewa mikopo wenzao wa mwaka wa kwanza mapema mwezi wa novemba


Chadema yapinga kuhusika na migomo vyuo vya elimu ya juu
Wakati hayo yakiendelea chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kimepinga shutuma zinazoletwa juu yake kuhusika na migomo vyuoni kama baadhi ya watu ambavyo husema,akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho Bwana Heche amesema,msingi wa tatizo lote ni bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo kila siku imekuwa ikilalamikiwa kuwa ndio chanzo cha matatizo,so serikali inabidi iwe makini katika kushughulikia masuala yanayohusu wanafunzi wa elimu ya juu na si kukimbilia kuwafukuza kwa tatizo ambalo chanzo chake kinaeleweka ni bodi ya mikopo!

1 comments:

  1. Tunaomba ututumie majina ya vijana waliofukuzwa ili 2wafahamu make unaweza kuta kijana wako nae yupo lakini akaamua kukaa kimya na kubaki mjini. fanya hivyo ili tujue nn cha kumshauri.
    mzee Butiku

Post a Comment